Uingereza yaifunga Hispania michuano ya Women’s Euro 2017

100

Timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza imefanikiwa kuifunga Hispania katika hatua ya mtoano ya kufuzu michuano ya Women’s Euro 2017 kwa jumla ya magoli 2-0.

Kikosi hicho cha Simba watatu kilifanikiwa kuwanza vyema mchezo huo wa kundi ‘D’ baada ya mchezaji wake Fran Kirby kuifungia timu hiyo goli la mapema huku Jodie Taylor akiifungia lapili katika kipindi chapili cha mchezo huo.

Katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Ureno imefanikiwa kuwafunga Scotland kwa jumla ya magoli 2-1 na hivyo kupata nafasi ya kusonga mbele.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wa kishangiria ushindi wao dhidi ya Scotland 2-1

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno anayechezea nafasi ya winga, Vanessa Marques amesema kufika hatua waliyopo sasa kwao ni historia na imewaongezea kujiamini zaidi kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Uingereza.

Kwa matokeo hayo timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza itacheza na Ureno katika mchezo wa mwisho siku ya Alhamisi wakati Hispania ikitarajiwa kuivaa Scotland.

Michezo ya kundi hilo lenye timu za Uingereza, Scotland, Hispania na Ureno itachezwa siku ya Alhamisi hii na kama Uingereza itashinda mchezo wake dhdid ya Ureno itatinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Mashindano hayo ya UEFA  Women’s Euro  yalianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1984 na Ujerumani kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza huku timu ya taifa ya wanawake ya Sweden ikiibuka na Ubingwa huo.

Na kwasa sasa bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya taifa ya Ujerumani ambao walilitwaa kombe hilo  Agosti 1 mwaka 2013, kwa mara ya sita.

 

Timu ya taifa ya Ujerumani wakishangilia Ubingwa wao mwaka 2013

Weka maoni