UN: tunatiwa wasiwasi na itikadi na wito wa chuki na vurugu Burundi

149
Vijana wa chama tawala "Imbonerakure" wakiwa kwenye moja ya maonesho

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inalaani uchochezi wa chuki na vurugu katika mikutano inayoendeshwa katika mikoa kadhaa ya Burundi. Kwa mujibu wa OHCHR, Imbonerakure, vijana kutoka chama tawala cha CNDD-FDD, lakini pia viongozi wa chama tawala au viongozi tawala wamekua wakitoa kauli hizo.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imenyooshea kidolea cha lawama viongozi hao kufanya kampeni ya kuwafanyia vitisho wananchi wa Burundi. Mamia ya vijana wa chama cha CNDD-FDD, Imbonerakure, mara kwa mara wamekuwa wakiimba nyimbo zinazotolea wito wa kuwapa ujauzito wanawake kutoka vyama vya upinzani na kuwaua wanaume wote kutoka vyama hivyo, bila hata hivyo kuchukuliwa hatua.

Gavana wa mkoa wa Makamba au rais baraza la Seneti, Reverien Ndikuriyo, mwenyewe pia alitoa kauli za kuchochea chuki.

Scott Campbell, mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, katika kanda ya Afrika ya kati, amesema “maneno haya ni ya kutisha na tuna wasiwasi kutokana na maneno haya, hasa katika eneo ambalo hujulikana sana kwa mauaji mengi yaliyotokea hivi karibuni“. Ameomba jumuiya ya kimataifa kutathimini kauli hizo. “Ni vizuri kuonyesha msimamo wetu sasa. Bila kukomesha ukatili, nchi inaweza kukumbwa na machafuko mabaya zaidi, ” amesema Scott Campbell.

Mapema mwezi Aprili, chama tawala cha CNDD-FDD, kililaani baadhi ya nyimbo hizo. Lakini Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inasema kuwa kampeni hizo zinaendelea bila wasiwasi wowoote. Gaston Sindimwo, Makamu wa rais, hajakanusha lakini amepuuzia mbali madai hayo.

Chanzo: RFI

Weka maoni