Vanessa Mdee adai hayuko tayari kupata mtoto sasa hivi..

189

Hit maker wa ngoma ya Kisela Vanessa Mdee kutoka Tanzania alikuwepo katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds fm kwenye exclusive interview kuzungumzia muziki wake na hata maisha binafsi.

Moja kati ya vitu ambavyo ameulizwa Vanessa Mdee ni kuhusu utayari wake katika suala zima la kupata Mtoto kwa kipindi hiki ukizingatia yeye ni msanii na vitu kama hivyo.

Vanessa Mdee amefunguka kuwa anandoto za kuja kuwa Mama siku za usoni, ila kwasasa hayuko tayari kabisa katika suala hilo.

“Natarajia kupata mtoto ila sio kwasasa, muda ukifika nitakuwa Mama ila kwasasa sina mpango wa kupata mtoto.” Alisema Vanessa Mdee.

Weka maoni