VIDEO: Manchester United yafungwa na Barcelona huko Marekani

137

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, Neymar Jr aameendeleza ubabe kwa kuichabanga klabu ya Manchester United goli 1-0 kwenye mchezo wa michuano ya International Champions Cup inayoendelea nchini Marekani.

Neymar aliipatia goli klabu yake ya Barcelona kunako dakika ya 31 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani.

Neymar of Barcelona gestures after scoring against Manchester United

Kwa matokeo hayo Manchester United wamemwagwa nje ya michuano hiyo yenye msisimko zaidi kwa kipindi hiki cha mapumziko (Pre-season).

Mchezo mwingine uliopigwa ni kati ya Juventus na matajiri wa Ufaransa, PSG ambapo matajiri hao wametupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigo cha goli 3-2.

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=z_JvWbzE7Gs]

Weka maoni