Viongozi wa soka Afrika Mashariki wapanga kuboresha soka

163
Jacques Tuyisenge wa Amavubi alifunga magoli wakati wakicheza dhidi ya Ethiopia katika michuano ya CECAFA mwaka 2015 (Picha/Timothy Kisambira)

Marais kutoka mataifa yanayounda Baraza la soka Afrika Mashariki CECAFA, wamekutana jijini Kampala kuzungumzia namna ya kuboresha mchezo wa soka katika ukanda huo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na marais kutoka mataifa saba ya CECAFA ambao ni pamoja na mwenyeji wao Moses Magogo, Vincent Nzamwita kutoka Rwanda, Jamal Malinzi (Tanzania), Juneidi Tilmo (Ethiopia), Nicolas Mwendwa (Kenya) na Ndikuriyo Reverien (Burundi).

Ravia Faina rais wa Shirikisho la soka katika kisiwa cha Zanzibar kilichopewa uanachama wa CAF hivi karibuni, pia alikuwepo.

Miongoni mwa mambo yaliyoafikiwa katika mkutano huo ni pamoja na:-

1 – Kuibadilisha Katiba ya CECAFA.
2 – Kuandaa mkutano mkuu wa CECAFA haraka iwezekanavyo.
3 – Kuhakikisha kuwa CECAFA inapata Makao makuu ya kudumu.
4 – Kuimaridha michuano ya CECAFA ya vijana chipukizi kwa viaja wasiozidi miaka 15, 17 na 20 kwa wavulana na wasichana pamojna na soka la ufukweni.

5 – Kuimarisha hali ya waamuzi, makocha, uongozi wa soka na kuimarisha afya kwa wachezaji.
6 – Kuimarisha mawasiliano na kuitangaza CECAFA.

7 – CECAFA kuomba nafasi ya kuandaa michuano ya bara Afrika katika siku zijazo.

8 – CECAFA kuwakilishwa ipasavyo katika Kamati kuu ya CAF.

9 – Kuja na mbinu za kuandika mapendekezo kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA ili kufadhili soka la vijana, wanawake na lile la ufukweni.

Chanzo: RFI

Weka maoni