Wachina 14 wakamatwa DRC kwa kufanya biashara haramu ya kuuza mbao

166
Miti iliyokatwa

Raia 14 wa Uchina wamekamatwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa madai ya kusafirisha mbao nje ya nchi hiyo, kinyume na sheria.

Maafisa katika jimbo la Katanga wamethibitisha kukamatwa kwa raia hao waliokamatwa wakikata miti katika misitu ya eneo hilo.

Serikali ya Uchina imesema inaunga mkono kukamatwa kwa raia wake, kwa sababu inaunga mkono uhifadhi wa misitu kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

Msemaji wa Wizara ya nje ya China Geng Shuang, amesema inaunga mkono jitihada za serikali ya DRC kuhifadhi misitu.

Hata hivyo, imeitaka serikali ya DRC pamoja na kuwakamata raia wao, kuhakikisha kuwa inaheshimu haki zao.

Serikali nchini DRC inasema hivi karibuni, tani 17,000 ya mbao zimesafirishwa hivi karibuni kwenda nchini China kupitia nchi jirani ya Zambia.

Chanzo: RFI

Weka maoni