Waliowaachisha masomo watoto Gicumbi mashakani

99
Bw Rwambukande Fidele

Mjenzi Rwambukande Fidele amepigwa faini ya faranga elfu 50 na kuonywa kwa makosa ya kukiuka haki ya mtoto wakati yeye ni mzazi.

Bw Rwabukwande amejitetea kwa kusema hakujua alichokifanya ni kosa, na kuongeza kuwa atahamasisha wajenzi wengine waondokane na kasumba ya kuwaajiri watoto.

Mkaguzi wa ajira wilayani Gicumbi, Karanganwa Jean Bosco amesema wamesimama imara kupambana na tatizo hili baada ya kusoma habari zilizoandikwa magazetini kulihusu.

Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha mara moja kuwapa vibarua watoto, akisema watoto wengi huacha shule kwa tamaa ya pesa atakayolipwa baada ya kufanya kazi.

Takwimu zinaonesha wiyalani Gicumbi kuna watoto 6,160 waliokatisha masomo na kujiingiza katika janga la kazi ngumu ikiwemo ufyatuaji matofali na uvunaji chai.

Weka maoni