Wasanii King James na Teta kutumbuiza Rwanda Day, Brussels

471
King James na Teta ni miongoni mwa wasanii wanaokubalika sana nchini Rwanda

Wanyarwanda kutoka nchi mbalimbali barani Ulaya wanajiandaa kumpokea Rais Paul Kagame atakayewahutubia kuhusu jinsi ya kuharakisha maendeleo ya Rwanda.

King James na Teta Diana ni miongoni mwa wasanii watakaowachangamsha Wanyarwanda hao, Brussels nchini Ubeljiji.

Wikiendi hii (Jumamosi) Rais Kagame anatarajiwa kutangamana na Wanyarwanda wanaomsubiri huko Brussels nchini Ubeljiji.

Wawili hawa siyo mara ya kwanza wanaalikwa kutumbuiza katika Rwanda Day kwani Teta mwaka jana alitumbuiza huko Amsterdam, King James alitumbuiza San Francisco.

Wawili hawa watashirikiana na wasanii wengine raia wa Rwanda waishio barani Ulaya ambao ni pamoja na Jali, Soul T bila kumsahau Ink.

Kila mwaka Rais Kagame huwatembelea Wanyarwanda waishio nje ya nchi yao hasa Barani Ulaya na Amerika, na siku hiyo ndiyo huitwa Rwanda Day kwa Kiingereza.

Licha ya rais Kagame kuelezea taswira ya maendeleo ya Rwanda na jinsi ya kuiboresha, Rwanda Day inakuwa ni nafasi nzuri kwa wajasiriamali kutangaza bidhaa au huduma zao.

Lengo la Rwanda Day inakuwa ni kuwahamasisha Wanyarwanda waishio nje ya nchi yao kushiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa lao.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Rwanda Day, hapa chini ni muktasari wa yaliyozungumzwa katika mikutano mbali mbali ya Rwanda Day tangu mwaka 2011.

Weka maoni