Watano wauawa Nairobi wakati wakimpokea Odinga

257
Amnesty International imelitaka Jeshi la Polisi liache mara moja kutumia risasi dhidi ya waandamanaji

Mwanasiasa wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema Jeshi la Polisi limetumia hadi risasi kuwatawanya wafuasi wake waliofurika kumpokea akitoka ughaibuni.

Maelfu ya Wakenya wameonekana mitaani wakifurahia msafara wa magari aliyowemo Odinga kutoka uwanja wa ndege wa Nairobi kuelekea Nairobi mjini kati.

Al Jazeera imeripoti vifo vya wafuasi watano wa Odinga katika zoezi la Polisi kuwatawanya.

Shirika la kimataifa la kupigania haki za binadamu la Amnesty International limeionya serikali ya Kenya dhidi ya kutumia risasi kudhibiti ghasia.

“Haivumuliki hata kidogo kutumia risasi kuyatawanya makundi ya watu,” amesema Abdullahi Halakhe, mtafiti wa shirika hilo Afrika Mashariki.

Hata hivyo, Polisi wamekiri kutumia gesi ya kutoa machozi na kukanusha kutumia risasi.

Jeshi la Polisi limesema watu watano waliuawa kwa kupigwa mawe na waandamanaji wenye hasira, baada ya kuonekana wakifanya vitendo vya uporaji.

Al Jazeera imesema wafuasi hao wa Odinga walikuwa wamefurika kwa wingi ili kusikia kutoka kwake baada ya siku nyingi akiwa nje ya nchi.

Weka maoni