Watu 15 wapotea kwa kuangukiwa na jengo la ghorofa saba Kenya

345
Watu waangukiwa na ghorofa Kenya

Usiku wa kuamkia Jumanne hii inakadiriwa watu wapatao 15 wamepotea baada ya kuangukiwa na ghorofa katika kijiji cha Kware Pipeline mtaa wa Embakasi, mashariki mwa mji mkuu wa Kenya – Nairobi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamelieleza gazeti la Star kuwa, Ghorofa hilo lilikuwa na dalili za kudondoka kwani lilikuwa na nyufa hata hivyo walifanikwa kuokoa watu kadhaa.

Pius Masai ambaye ni Mratibu wa shughuli za uokoaji ameeza kuwa watu wapatao 100 wamejeruhiwa ila idadi inaweza kuongezeka. Hata hivyo familia 121 zilizokuwa zikiishi katika jengo hilo zilihama kabla ya maafa hayo, kwa mujibu wa Bongo5.

Jeshi la polisi nchini humo likishirikiana na Shirika la msalaba mwekundu wanaendelea na juhudi za kuwatafuta waliopo katika jengo hilo.

Weka maoni