Waziri Mwigulu atishia kuwafuta uraia Watanzania Wapya mkoani Katavi

119

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ametishia kuwafuta uraia Watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao walikuwa wakimbizi kwa muda mrefu waliotokea nchini burundi wakati wa vita ya kikabila miaka 1972

Amesema hayo akiwa ziarani mkoa wa katavi kutembelea kambi ya katumba ambayo wamepewa uraia wa Tanzania na kupitia kambi zingine kuangalia usajili unaendeleaje. Waziri Mwigulu amechukizwa na tabia ya baadhi ya wananchi waliopata uraia kubaguana kitaifa na kikanda ambapo inafikia mahali hawanunui bidhaa kutoka kwa mwingine ambaye si wa kutoka ukanda wake.

Waziri Mwigulu amewaambia kuwa yoyote atakayeleta mambo ya ubaguzi katika jamii hatosita kumfutia uraia alioupata kwani Watanzania hawana mambo ya kibaguzi.

Waziri Mwigulu pia amewataka Watanzania kuwa na utanzania ndani ya mioyo yao na waache tabia ya kutaka kukwamisha kila kitu kinachofanywa na serikali basi wao ni kuweka vikwazo mbele kisifanikiwe.

 Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema amewataka watanzania hao wapya wapeleke watoto nje ya maeneo hayo hata mikoani ni ruksa kwani wao wanahaki sawa kama watanzania wengine wasiwe na tatizo lakini amewataka wasibadilishe majina.
Wananchi zaidi ya 7000 kati ya laki mbili bado hawajachukua hati zao za uraia mpaka sasa lakini teyari zimekaamilika mda mrefu.​

Weka maoni