Will Smith amepata shavu ndani ya Disney

141

Kama wewe ni moja ya wahenga ambao ulipata nafasi ya kutazama cartoon ya Aladdini, Sasa kao mkao wa kula kuipokea toleo jingine la Aladdin ambalo Will Smith ametajwa kupewa shavu la kutumika kama  Genie.

Kama umepoteza kumbukumbu Genie ni nani, Genie ni ule kama mzimu ambao unatoka mule kwenye ile birika la kimijiuza baada ya kuisugua mara tatu na kukupa nafasi ya kutimiza wish zako tatu baada ya hapo anakuwa huru.

Image result for aladdin movie

Baada ya kuwa na mafanikio mazuri katika filamu yao ya Beauty and Beast, Disney wamepanga kuzirejesha cartoon zake za kitambo katika ulimwengu wa sasa wa filamu ambao cartoon kama Dumbo na Mulan, kupitia  Rolling Stone wametoa taarifa kwamba script ya filamu hiyo imeandikwa na John August ambapo filamu hiyo inatajwa kuongozwa na Guy Richie.

Weka maoni