X-Dirhor atishia kusambaza video ya Jay Polly akifanya ngono na kahaba mkimbizi

X-Dirhor ameshafunguliwa mashtaka baada ya kumhusisha Jay Polly na kashfa ya ngono ambayo inaweza kumsababishia mazingira mabaya kwenye muziki na kwenye ndoa yake pia.

663
Tuyishime Joshua maarufu kama Jay Polly, msanii wa Hip Hop nchini Rwanda

Ndagijimana Eric almaarufu X-Dirhor ambaye anajulikana katika shughuli za uandaaji wa matamasha ya muziki nchini Rwanda, ametishia kutoa video ya ngono ya rapa Jay Polly.

Amesema ataachia video hiyo ili kulipiza kisasi na kulazimisha kulipwa faranga laki tatu aliyodhulumiwa na Jay Polly baada ya kumpa dili la faranga miliyoni moja.

Amesema anayo video ya mwanamuziki huyo akifanya mapenzi na kahaba ambaye ni mkimbizi wa kirundi katika hoteli ya Golden Monkey wilayani Nyamagabe alikokuwa amekwenda kutumbuiza.

“Ninachotaka ni kwamba anilipe pesa yangu vinginevyo nitamuanika watu wote waione hiyo video” amesema X-Dirhor akizungumza na Habari Pevu.

“Nimeamua kutoa siri zake baada ya yeye kunidharau, nilimdai akawa ananiambia nifanye ninachokitaka, eti anajua jina lake ni kubwa sitaliathiri kivyovyote.”

Alipoulizwa jinsi alivyochukua video hiyo, amesema hiyo ni siri yake asiyoweza kuzungumzia. “Hilo siwezi kulizungumzia ila video ninayo na anajua ninayo,” amejibu kwa msisitizo.

X-Dirhor amesema waliingia mkataba wa kumlipa faranga 350,000 ya udalali baada ya kumsaidia kupata kibarua cha faranga miliyoni moja kutoka RGB (Mamlaka ya Uongozi Bora Rwanda) katika kampeni ya Nk’uwikorera inayolenga kupiga vita utoaji mbovu wa huduma nchini, na baada ya tamasha kufanyika aliishia kumlipa elfu 50 tu.

“Hakujua nina video hiyo mpaka nilipomuambia mwenyewe, akitaka tupelekane kizimbani kisa nimesambaza video hiyo sijali, niko tayari kwa lolote, kanifanyia maovu, ninachotaka ni hela yangu anilipe mambo yaishe.”

X-Dirhor

Alipoulizwa kama kuna marafiki wa Jay Polly aliowaelezea mvutano baina yao ili wawasaidie kupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, amesema hakuwa na haja ya kufanya hivyo kwa kuwa hata waliokuwa maswahiba wake wamemwagana baada ya yeye kuwadhulumu pia.

“Anajifanya mjuaji sana, angeniambia kwamba ameshindwa kunilipa ningemuelewa ila ubaya wake ukimdai analeta nyodo kana kwamba huwezi kumfanya chochote,” ameongeza.

Jay Polly akanusha kufanya ngono na mkimbizi

Jay Polly ambaye ni miongoni mwa wawakilishi mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini Rwanda, amekanusha madai ya kufanya ngono na mkimbizi akiyataja madai ya X-Dirhor kuwa ni mkwara.

“Kama anayo video mbona haitoi? Anadanganya, sijaingia mkataba naye na wala sijafanya mapenzi na mkimbizi, ni uongo tu ametunga kwa lengo la kunidhalilisha. Tumekuwa tukiona watu wakitengeneza picha kwa photoshop sasa kama ana video si aisambaze tuione?,” amesema Jay Polly akizungumza na Habari Pevu.

“Nimeshamfungulia mashtaka, manasheria wangu amefanya hivyo naamini kuna mabaya mengine yanaendelea nyuma ya pazia ukweli utadhihirika.”

Rapa huyu amemuelezea X-Dirhor kuwa ni mhuni anayetapatapa na dunia, ambaye hawezi kumtafutia msanii kibarua kama anavyojigamba wakati hata yeye hajiwezi.

“Mzururaji huyo, hajawahi kunitafutia kibarua anatafuta kiki tu mjinga huyo.”

Alipoulizwa kama madai haya ya yeye kuhusika katika kashfa ya ngono hayatamchafulia jina ukizingatia ni msanii mkubwa na ambaye ana mke na watoto, haya ndiyo majibu aliyotoa: “Hata wachungaji wa makanisa huongelewa, maadui wapo.”

Amesema X-Dirhor yupo kwenye genge la wazinguaji ambao wanamchafulia jina katika juhudi za kukwamisha wimbo wake mpya uitwao ‘Nta mpaka’ ambao amesema utatoka leo.

Jay Polly ni miongoni mwa nguzo muhimu za muziki wa Hip Hop nchini Rwanda. ‘Ndacyariho ndahumeka’, ‘Oh My God’, ‘Rusumbanzika’, ‘Akanyarirajisho’ ni miongoni mwa ngoma zilizomzolea umaarufu.

Wazo moja

  1. Huyu X-Dirhor namuomba aisambaze hiyo video awe mstaarabu, kama anajua alidhulumiwa si aende mahakamani? Akisambaza hiyo video yeye ndo atatupwa jela, kwa hiyo atumie busara asikurupuke la sivyo atakuwa na majuto kama ya ma Pharaohs

Weka maoni