Zione picha za rapa Ciney akifunga ndoa na mpenzi wake

405
Ciney akiapa kuwa mke mwaminifu huku mumewe akiwa amemshikia mic

Msanii wa kike wa muziki wa Hip Hop nchini Rwanda Uwimana Aisha maarufu kama Ciney na mpenzi wake aitwaye Tumusiime Ronald  wamefunga ndoa ya kiserikali leo Ijumaa.

Tukio hilo la kufunga pingu za maisha limefanyika katika Tarafa ya Kimihurura, Wilaya ya Gasabo Jijini Kigali, ikiwa ni baada ya kuona mapenzi yao yamenoga kwa kudumu kwa zaidi ya miaka minne.

Tumusiime ameahidi kumpenda Ciney kwenye raha na dhiki mpaka mwisho wa maisha yake

Ciney amekaririwa na Igihe akidai kwamba baada ya ndoa ya kiserikali wanajiandaa kwa ajili ya ndoa ya kidini itakayofanyika mnamo Julai, 2017 katika Kanisa la Kianglikani.

Ciney akiwa anamsikiliza kwa makini katibu mtendaji wa tarafa aliyewaoza
Katibu mtendaji wa Tarafa ya kimihurura amewaelezea kinagaubaga maharusi hawa kuhusu maisha ya ndoa

Mwanamuziki huyo alivishwa pete ya uchumba miezi miwili iliyopita.

Huyu ndiye mwanaume aliyejihakikishia moyo wa Ciney

Majuzi Ciney alijiunga na Kanisa la Kianglikani la Biryogo lililoko Kigali mjini kati, ambalo ndilo wataozwa.

Maharusi na marafiki zao wakimsikiliza kwa makini mtendaji wa tarafa aliyewaoza huku wakitabasamu

Ciney amesema kadi za mwaliko wa harusi zitatoka katika siku za hivi karibuni.

Hawa ni miongoni mwa wanafamilia wa Tumusiime Ronald

‘Nkunda’, ‘Igire’ ‘Ngwino Nkwereke’ ni miongoni mwa ngoma zake zilizopendwa.

Picha: Igihe

Wazo moja

  1. Mgaya wa Tabora, ningependa kujua mengi kumhusu huyu mwanamke, nimeusikiliza huo wimbo wake upo poa japo sijaelewa hicho kilugha anamaanisha nini. Namtakia ndoa ya amani na furaha

Weka maoni